JAMAL
Emil Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani
Jumanne Nyamlani.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es
Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa
kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega
sita. Katika
nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred
Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir
kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.
Kanda
ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki
Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid
Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63,
huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati JamesMhagama
aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya
nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.
Kanda
ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo
aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya
19 za Ally Mtumwa.Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai. Mbasha
Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61,
wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati
kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda
namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.
0 Comments