![]() |
![]() |
Masogange akipozi na Jack Patrick. |
Masogange
ambaye siku ya tukio alikuwa na nduguye, Melisa Edward baada ya kunaswa
na madawa hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo
uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo alihukumiwa kwenda
jela miezi 32 au kulipa faini ya shilinghi milioni 4.8 ambapo aliweza
kulipa na kuwa huru.
Tangu aachiwe huru, Septemba mwaka huu,
msanii huyo akawa hajulikani alipo huku baadhi ya ‘posti’ zake kwenye
mtandao wa kijamii wa Instagram zikionesha yupo Tanzania au Afrika
Kusini.
![]() |
Masogange akipozi dukani Bongo.
Jumatatu
iliyopita, mida ya saa kumi jioni, paparazi wetu alipigiwa simu na
msomaji wa gazeti hili (jina tunalo) akisema amemwona Masogange akiingia
kwenye duka la nguo lililopo Sinza Kamanyola, Dar akiwa peke yake.
Paparazi
wetu alijipanga kwa kamera na kutia timu kwenye duka hilo ambapo hata
hivyo muuzaji alisema aliondoka baada ya kufanya manunuzi ya kawaida.
Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.
Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.
Jack
alipigiwa simu ambapo alikiri kuwa na Masogange siku ya Jumanne kwenye
duka hilo. Akasema: “Mimi nilimkuta pale, tukapiga picha tukaachana,
basi.”
Kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi, Masogange
alipatikana na kukiri yupo Dar lakini akasema hakutaka kuweka wazi kwa
sababu anawaogopa sana mapaparazi.
0 Comments