Mganga mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ramadhan Kabala akizungumza katika viwanja vya Shy-com |
Imeelezwa kuwa wanawake mkoani
Shinyanga wanaongoza kwa kuwa na uzito mkubwa ukilinganisha na wanaumme,
hali ambayo inaashiria kuwa na magonjwa sugu yasiyoambukizwa ukiwemo ugonjwa wa
kisukari kutokana na mrundikano wa mafuta mwilini.
Hayo yamesemwa jana na Mganga mkuu wa
Hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ramadhani Kabala, wakati wa maadhimisho ya
siku ya kisukari duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Shy-com
mjini Shinyangaa.
Dkt Kabala amesema utafiti
uliofanywa na ofisi yake kwa kushirikiana na shirika la Bima ya
afya umeonesha kuwa 35.6% ya wananchi wa Shinyanga wenye umri kati ya
miaka 15 hadi 80, wana uzito mkubwa kuliko urefu wao.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kati ya
watu hao 23% ni wanaumme na 52.4% ni wanawake,
na kwamba 22.9% ya watu wenye umri chini ya miaka 45 wana uzito mkubwa wakati
wenye umri zaidi ya miaka 45 ni 12.8% tu.
Dk Kabala amesema hadi sasa asilimia
5.2 ya wananchi wa Shinyanga wanaugua ugonjwa wa kisukari, ambapo wanaumme ni asilimia
45 na wanawake ni asilimia 6.1.
Dkt Kabala amesema ugonjwa wa
kisukari unasababishwa na kunywa vinywaji vilivyosindikwa kwa wingi, vinywaji
vyenye sukari nyingi, kula vyakula vilivyokombolewa na vyakula vyenye mafuta
mengi bila kufanya mazoezi.
Naye mgeni rasmi katika maadhimisho
hayo, ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga amewataka wananchi kupima
afya zao mara kwa mara, kuepuka ulaji mbaya, na kufanya mazoezi kwa muda wa
nusu saa kila siku.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akitoa hotuba!! |
Rufunga amesema kwa mujibu wa Shirika la
Afya duniani (WHO,2002), zaidi ya watu milioni 347 duniani wana kisukari na
asilimia 80 wanatoka nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na waathirika wakuu ni
wenye umri wa miaka 40 hadi 59.
Maadhimisho ya siku ya kisukari
duniani, Mkoani Shinyanga yametanguliwa na maandamano ya kutembea kwa kasi kama
njia ya kufanya mazoezi, huku yakiwa na Kauli mbiu ya Tujikinge na tuikinge
jamii ijayo na ugonjwa wa kisukari”.
TIZAMA MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Annarose Nyamubi akimkaribisha mkuu wa mkoa wa shinyanga |
Kushoto mwenye jaketi ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Anna Rose Nyamubi akitembea wakati wa maandamano ya leo katika siku ya kisukari duniani Novemba 14 mwaka 2013 |
Wanafunzi wa shule za sekondari nao walikuwepo katika maadhimisho hayo yaliyoongozwa kwa kauli mbiu-TUJIKINGE NA TUIJENGE JAMII IJAYO NA UGONJWA WA KISUKARI |
Kikundi cha watafuta njia(Pathfinder club) kutoka kanisa la Waadventista Shinyanga wakimpokea mkuu wa mkoa katika viwanja vya Shy-com pamoja na kuonesha gwaride lao |
Maafisa wa ulinzi na usalama nao walikuwepo |
Msafara wa maandamano ukiingia uwanjani,hao ni baadhi ya madaktari na wauguzi kutoka hospitali ya mkoa wa shinyanga |
Mbele ni Kiongozi wa kikundi cha Watafuta njia akimwongoza mkuu wa mkoa eneo la jukwaa kuu |
Ilikuwa ni furaha mwanzo mwishoooooo |
0 Comments