MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Kwezi Seleli (20) mkazi wa kijiji cha Kalama,kata ya Uyogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuwawa kwa kuchinjwa sehemu za shingoni na mume wake akiwa amelala usiku.
![]() |
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Evarist Mangala |
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Evarist
Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo saa kumi alfajiri
katika kijiji hicho huku akimtaja mwanamume aliyefanya mauaji hayo kuwa
ni Chalia Samweli (25).
Kwa mujibu wa Kamanda huyoa amesema kuwa mwanaume huyo alitumia
panga kumuua mke wake huku naye akifanya jaribio la kujia kwa
kunywa sumu aina ya Diazone inayotumika kuogeshea mifugo ambapo hakufa
alikuwa mahututi.
0 Comments