
Mwanamke
huyo aliyetambulika kwa jina 'Grace Wambui', Alimueleza Hakimu 'Enyara
Emukule' wa mahakama kuu kwamba alimshindilia vidonge hivyo vya usingizi
mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja ili alale usingizi mzito asimkere
kwa kulialia.
Ilmradi
apate nafasi ya kutoka na wanawake wenzie ambao walikuwa wakijihusisha
na biashara ya kuuza mwili (Uchangudoa) lengo likiwa nikutafuta pesa za
kujikimu kimaisha kwa kuwahudumia watoto wake wengine wakubwa zake na
huyo aliyemezeshwa vidonge.
Lakini
kwa bahati mbaya baada ya kukamilisha zoezi hilo alielekea moja kwa
moja mihangaikoni na kujipatia vijisenti vya kujikimu kama kawaida, Sasa
basi..! Siku ya tukio Grace Wambui alipotia maguu nyumbani kwake
alikuta majirani wamejazana top! Kumbe maskini wa mungu yule kiumbe
ameaga dunia kupitia vidonge vya usingizi alivyomshindilia.
Kumbe
majirani walishapiga simu polisi..!,Huku na kule akashangaa polisi
wametia timu na kumtia mbaroni mpaka sasa anasubiria kusomewa mashtaka
Wiki Ijayo.
0 Comments