Advertisement

Responsive Advertisement

AL AHLY YAIONDOA YANGA KOMBE LA MABINGWA AFRIKA KWA MIKWAJU YA PENALTI

 
Na Baraka Mpenja 
BAHATI haikuwa kwa Yanga usiku huu. Wametolewa na Al Ahly kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika kuwania hatua ya 16 bora baada ya kufungwa bao 1-0 ndani ya dakika 90.
Mabingwa watetezi, National Al Ahly wamepata penati 4  huku Young Africans wakipata penati 3.
Waliofunga penati za Yanga ni  Didier Kavumbagu `Kavu`, nahodaha na beki wa kati, Nadir Haroub `Canavaro`,  na Emmanuel  Anord Okwi .
Wanandinga wa Yanga waliokosa penati usiku huu ni Oscar Samwel Joshua , Said  Bahanuzi na Mbuyu Twite .
Mlinda mlango namba moja wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ alipangua penalti mbili mfululizo ya nne na ya tano, lakini Yanga SC nao wakakosa penalti mbili mfululizo ya nne na ya tano.
Mbali na kupangua penati hizo, alicheza vizuri ndani ya dakika 90 na kuwa kikwazo kikubwa kwa Al Ahly kupata ushindi.
Mchezo wa leo umemalizika kwa Yanga kufungwa bao moja sawa na matokeo waliyoyapata Yanga katika mechi ya kwanza jijini Dar es salaam, Machi mosi mwaka huu uwanja wa Taifa.
Al Ahly wanapata penati 4 - 3 Young Africans
Waliopata Yanga Didier, Canavaro, Okwi huku waliokosa ni Oscar Joshua, Said Bahanuzi na Mbuyu Twite, kutokana na matokea hayo klabu ya Al ahly ya Misri wanafuzu hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa Afrika.
Categories:

Post a Comment

0 Comments