


Watu 19 wa kijiji cha Utaho, wilayani Ikungi mkoani Singida jana wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne
wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa
wanatoa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliyegongwa na
gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja jana usiku.
Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-Salaam.
Taarifa zinasema Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Mwandishi wa habari Elisante Mkumbo alifika
na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa katika kituo cha polisi cha
Ikungi bila ya kujua hatima yao ya safari baada ya basi lao kuwakanyaga
na kuuwa watu 19.
0 Comments