Hemedy PHD na King Majuto wapo jijini Mwanza kushoot filamu yao mpya ya comedy iitwayo ‘Kimbulu’. Hemedy ameiambia BK kuwa uamuzi wa kufanyia filamu hiyo jijini Mwanza
ni kutaka kupata mazingira tofauti kwakuwa filamu nyingi za Tanzania
hufanyika jijini Dar es Salaam.
Hemedy kama mwizi wa kuku “Watu wengi wamekuwa wakisema kwamba wamechoka kila siku kuona
majengo ya Dar es Salaam kwahiyo tumeamua kubadilika kuja huku halafu
Mwanza yenyewe sio town ni kidogo nje ya mji. Nafikiri kutokana na
mandhari ya Mwanza mawe mawe mtu atakuwa anajua kabisa kwamba project
hii imefanyika ndani ya Rock City,” amesema.
Wanakijiji wakimfanshambulia Hemedy Akisimulia mkasa wa filamu hiyo, Hemedy amesema inawahusu vijana
wawili wanatoka mjini wanakwenda kijijini kutafuta waigizaji wa filamu
ili wawaunganishe na mastaa wakubwa wa filamu lakini wanapofika huko
mambo hayaendi kama walivyokuwa wanatarajia na kujikuta wakifanya uzinzi
tu. “Kwahiyo inafika stage sasa kijiji kinajua tabia zetu mbaya
tunawindwa sana na yule mzee mwenyewe ambaye ni babu yetu tulipofikia na
yeye tabia yake hizohizo halafu anaentertain. Kwahiyo sisi tukipiga
vitoto yenyewe anapiga wake za watu mpaka mwisho wa siku tunakuwa wezi
kijijini kule,” ameongeza. Hemedy akiwa na wakazi wa location ya jijini Mwanza wanakoshoot filamu mpya. Hemedy amesema lengo la filamu hiyo ni kuonesha hali halisi ilivyo
kwenye tasnia ya filamu ambapo watu wengi hurubuniwa na matapeli. “Kwahiyo ni kuwafungua macho wale wote wanaotumika kwa style hiyo na
vilevile kuonesha wasanii kwamba kama tunaamua kusaidia tusaidie kweli
na isiwe watu tunawafanyia michezo mibaya kama hiyo.” Katika hatua nyingine, Hemedy amesema hataki kushirikishwa kwenye tuzo za Action n Cut. “I really appreciate kwa wale waliohisi nafaa kuingia kwenye hizi
tuzo hasa category ya best actor…ILA SIONI SABABU YA MASHABIKI ZANGU
KUPOTEZA MUDA NA PESA ZA KUVOTE KWANGU!!!……IM NOT INTERESTED!!!…..TUZO
YANGU IPO KWA MASHABIKI ALWAYZ.AND IM SO PROUD OF WHAT I
DO!!!!…#PAPPINATION,
0 Comments