Mwenyekiti
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe (kulia) na Mjumbe
wa Umoja huo, James Mbatia wakiingia katika Ukumbi wa African Dream
mjini Dodoma walipohudhuria mkutano wa wajumbe wa Bunge la Katiba wa
umoja huo ambao wamegoma kuendelea kuhudhuria vikao vya Bunge.
Ni baada ya kuchelewa kuwasili katika mkutano wao, walihofia kugeukwa baadaye aliwasili na kuwaeleza yaliyojiri. Wajumbe
wa Mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), juzi nusura
wamgeuzie kibao mwenyekiti wao, Freeman Mbowe baada ya kuchelewa kufika
kwenye mkutano ulioandaliwa ikiwa ni siku moja baada ya kususia kikao
cha Bunge la Katiba.Ukawa walikutana kwenye Ukumbi wa African Dream kwa ajili ya kujipanga baada ya kususia mkutano wa Bunge. Mkutano huo ulioanza saa 4:18 ukiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba baadaye wajumbe walianza kuhoji walipo viongozi wao, Freeman Mbowe na James Mbatia.Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Profesa Abdallah Safari alisimama na kuhoji walipo viongozi hao hatua iliyoanza minong’ono miongoni mwa wajumbe wakiwa na hisia kwamba huenda wamewageuka na kwenda kwenye Kikao cha Kamati ya Uongozi.“Tujue kabisa kama wametugeuka.
0 Comments