Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque
amesema hana njia ya mkato ya kusema samahani kwa mashabiki wa soka wa
nchi hiyo kufuatia kikosi chake kushindwa kuonyesha uwezo wa kutetea
ubingwa wa kombe la dunia.
Vicente del Bosque amesema kikubwa anachokiona mbele yake ni kukubaliana na hali halisi iliyoonekana tangu waliponza kampeni ya kutetea ubingwa wao juma lililopita, kwa kufungwa mabao matano na Uholanzi na kisha kupoteza mbele ya timu ya taifa ya Chile.

Amesema kikosi chake hakikucheza vizuri tangu mwanzoni mwa fainali za
mwaka huu, na hali hiyo imekuwa dhambi kubwa sana kwao na kujikuta
wakiondolewa mapema tofauti na ilivyokuwa inafikiriwa.
"Hatuna sababu za kujitetea, zaidi ya kukubaliana na hali iliyoonekana
uwanjani tangu kwenye mchezo wa kwanza," amesema del Bosque.
"Kikosi changu kimecheza chini ya kiwango tangu dakika ya kwanza ya
mchezo dhidi ya Chile, na matokeo yake tumeambulia adhabu ya kufungwa
mabao mawili kwa sifuri yanayotutupa nje ya michuano hii’’ Ameongeza
kocha huyo.
Kwa upande wake mlinda mlango pamoja na nahodha wa timu ya taifa ya
Hispania, Iker Casillas amesema ni vigumu kuamini kilichotokea uwanjani
hapo jana, lakini hawana budi kukubaliana na hali hiyo ambayo ulimwengu
mzima imeiona.
0 Comments