MJASIRIAMALI na mwigizaji wa sinema za Kibongo,
Illuminata Poshi ‘Dotnata’ ameibuka na kusema anachukizwa na watu wenye
kasumba ya kumsema vibaya mwigizaji Wema Sepetu ‘Beutiful Onyinye’,
waache.
Akipiga stori na paparazi wetu Dotnata alisema anakerwa sana na watu
wanaokuwa na chuki na mwigizaji huyo ambaye yeye anamchukulia kama lulu
katika tasnia ya uigizaji.
Mjasiriamali na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’.
“Siwapendi wanaomchukia Wema ambaye mimi huwa namuona kama
nyota katika sanaa, wamuache mtoto wa watu afanye kazi zake, si watafute
kazi za kufanya kuliko kumuongelea mabaya,” alisema Dotnata pasipo kuwataja majina watu hao.

0 Comments