
Shabiki makini: Mchumba wa Mario Balotelli, Fanny Neguesha alikuwa miongoni mwa mashabiki wa Italia dhidi ya England.
MSHAMBULIAJI mtukutu, Super
Mario Balotelli macho yake hayakuwa kwa taifa lake tu, bali hata kwa
mchumba wake Fanny Neguesha ambaye alikuwa miongoni mwa mashabiki
waliofurika katika mchezo wa ufunguzi wa Italia wa kundi D dhidi ya
Simba watatu, timu ya taifa ya Engaland.
Katika mechi hiyo ambayo
Balotelli aliifungia Italia bao katika ushindi wa 2-1, mchuchu wa nyota
huyo alivalia jezi namba 9 ya Italia yenye jina la basha wake,
Balotelli.
Neguesha kwa muda wote alikuwa
na tabasamu baada ya mpenzi wake kufunga bao safi kwa kichwa mapema
kipindi cha pili na kuifanya Italia iwe mbele kwa mabao 2-1.

Mambo safi!: Neguesha akifurahia hali ya hewa mjini Manaus na kupiga picha kwa simu yake.

Tabasamu tupu: Neguesha akipunga mkono kwenye screen kubwa ya uwanjani wakati Italia ikiiadabisha England.

Mmiliki wa `totoz zuri`:
Balotelli (katikati) alianza katika kikosi cha Italia kwenye mechi ya
ufunguzi dhidi ya England mjini Manaus

Rasmi: Balotelli alitangaza kumchumbia Neguesha kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram jumatatu ya wiki hii.
0 Comments