Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Geita Kamishina Msaidizi Josephu Konyo Akionyesha Bunduki Aina Ya SMG Iliyokuwa Inatumiwa Na Majambazi hao |
WATU
wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuwa jana jioni wilayani
Nyang’hwale mkoani Geita kwa tuhuma za kumvamia na kumua Mfanyabiashara
wa M-Pesa Gosbert Kulwa(59) katika eneo la benki ya NMB mjini Geita
kisha kukimbilia Nyang’hwale.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita Joseph Konyo amewambia waandishi wa habari kwamba jana saa 11.30 jioni watuhumiwa hao walimvamia Marehemu Kulwa na kumpiga risasi tumboni ambapo baadaye alifariki wakati akitibiwa katika Hospitali ya wilaya ya Geita.
Konyo amesema baada ya kutenda unyama huo wahalifu hao walipokonya kiasi cha pesa kisichojulikana na kukimbia kwa pikipiki aina ya sanlg yenye nambari za usajiri T-460-CVQ, kuelekea kwenye pori la kijiji cha Ibambila wilayani Nyangh’hwale.
Amesema, kabla wahalifu hao hawajamvamia Marehemu Gosbert walianzia kwa mfanyabiashara wa vinywaji Ignas Atanas waliyempokonya Bastora aina H PIETRO BERRETA HO4788Y waliyokutwa nayo wakati wakifuatiliwa na kiasi cha pesa ambacho pia hakikufahamika.

Majambazi
hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi
walikamatwa wakati wanakimbia ambapo mmoja alijaribu kujihami kwa
kurushia askari risasi kabla yas kugongwa kwa gari na dereva shupavu wa
jeshi la polisi.
Imelezwa, jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askali wakaanza kumfukuza wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa kumkamata na kuanza kushambuliwa kabla ya kufariki wakati anakimbizwa kupelekwa hospitalini.
Wananchi wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya tukio hilo kutokea huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi nhilo ili kuimarisha amani katika mkoa huo.
Wananchi Wa Mjini Geita Waliofulika Katika Hosptari Ya Wilaya Ya Geita Wakiangalia Miili Ya Majambazi hao |
Na Valence Robert - Geita
0 Comments