Serikali ya Uganda imekifungia kituo kikubwa cha Televisheni cha nchi hiyo NTV kuripoti habari zozote zinazomhusu Rais baada ya kurusha hewani picha zinazomuonyesha Rais Yoweri Museveni amesinzia bungeni.
Mkurugenzi wa kituo cha habari za serikali Dennis Katungi amenukuliwa
akisema: “Rais ana tabia zake wengi mnajua, huwa anatafakari na
wanajua lakini bado wameonyesha picha hizo na kusema alikuwa amesinzia.”
Msemaji wa serikali Ofwono Opondo amethibitisha kuwa NTV Uganda
itachukuliwa hatua za kinidhamu ambapo wameifungia kuripoti habari
zozote zinazomhusu rais wakati bado serikali ikiangalia uhusiano wake na
chombo hicho.
Ameituhumu NTV kwa kukosa utaalamu wa uandishi na kuegemea upande
mmoja lakini hata hivyo hatua hiyo si ya kudumu ni ya muda tu kuwafanya
wafikirie upya.

0 Comments