Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa
hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya
wokovu.
Akizungumza na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa
anapata shida sana kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila
anachofanya watu wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza vitu vingi sana
kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa jicho
linginewanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya kuokoka?
Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si mlokole,
siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda

0 Comments