Marekani imeadhidhibu Uganda kwa kuweka sheria kali ya kupinga mapenzi ya jinsi moja katika taifa hilo.
Msemaji
wa Whitehouse, Caltlin Hayden ameeleza katika barua yake kwa vyombo vya
habari kuwa sheria iliyopitishwa na bunge la Uganda ikiuka haki za
binadamu.
Vikwazo
vya Marekani kwa Uganda kama adhabu, vinajumisha kuwapiga marufuku
wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kutoingia Marekani.
Marekani
itapunguza ushirikiano na Wizara ya Polisi na Afya za Uganda, na
kuachana na mpango wa mazoezi ya kijeshi kati ya wanajeshi wa Marekani
na wanajeshi wa Uganda.
Uganda
walipitisha sheria ambayo inaeleza wazi mtu atakayekutwa na hatia ya
kushiriki katika masuala ya ushoga atahukumiwa kifungo cha maisha jela.

0 Comments