Mkali
wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa kuvunja (dancer) amezungumzia
uhusiano wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya.
Msami alizunguka sana mbuyu kutaka kutoa
maelezo kuhusu ukweli wa mambo kati ya wawili hao lakini kwa mara ya
kwanza aliamua kuiambia Times Fm kauli yake kutokana na jinsi
alivyoulizwa.
“Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach ili apate jibu. Ni kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha.” Amesema Msami..
Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa muonekano uliwafanya wengi
wazungumze kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami amegeuka Serengeti Boy
kwa Uwoya ambaye wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli ni kwamba
Msami ni mkubwa kwa Uwoya.
“Unajua mimi mwanzo, Serengeti
Boy nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Yaani ile deeply nilikuwa
sina tafsiri yake kabisa yaani. Kwa hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake
‘Serengeti Boy’ kumbe ni mtu ambaye amezidiwa umri. Tofauti na mimi
nilivyokuwa nawaza kuhusu Serengeti Boy.
“Lakini mbona nikasema kama ni
hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi
umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi
ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi
mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya.” Amesema Msami
Katika hatua nyingine, Msami ameeleza mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.
Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye mhusika mkuu na kwamba ni filamu ambayo itahusisha dance na muziki.
Filamu hiyo itatoka mwaka huu lakini bado haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.
“Movie inakuja very soon, watu wakae tayari.” Amesisitiza.

0 Comments