Mwanamuziki Hafsa Kazinja.
Mwanamuziki Hafsa Kazinja anayetamba na Wimbo wa Mlala Nje huku video yake ikiwa tayari, ameamua kuikacha dini yake ya Kiislam na kuhamia kwenye Ukristo.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hafsa alisema alifikia uamuzi huo baada ya kusumbuliwa na maruhani ambayo yalimfanya arukwe na akili.
“Niliumwa sana hadi ikaonekana
nimerukwa na akili, maruhani ndiyo yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi
yalikuwa yakiniambia nisile samaki wala dagaa, mara yakaniambia
natakiwa kuwa mganga.
“Njia zote ziligonga mwamba,
nikaambiwa nisali na nimuachie Mungu, nikawa nikisali sauti zinanijia
nimtukane Mungu tena matusi makubwa, nimeenda hadi kwa waganga, mashehe
na walokole wakaniombea na nikapoteza pesa nyingi hadi nikauza nyumba
yangu na magari lakini wapi. Nimekwenda Kanisa la Zoe ndiyo nimepona,
namshukuru Mungu.
AAMUA KUOKOKA
“Sasa nimeamua kuwa Mkristo, yaani nimebadili dini kwa
kumaanisha, nampenda Mungu katika roho na kweli. Sijabatizwa hivyo bado
sijabadili jina ila nasali Kanisa la Zoe lililopo Segerea jijini Dar.”

0 Comments