Msanii wa filamu za vichekesho, Salma Jabu aka Nisha anatarajia kuachia wimbo wa "Gumzo" aliyomshirikisha Mzee Majuto.
Kwa
mujibu wa tovuti ya bongo5 Nisha amesema kuwa ameamua kuachia wimbo
huo ili kuwaridhisha mashabiki wake baada ya kumtaka hautoe wimbo huo.
'Kuna kipande cha wimbo nilikiimba kwenye filamu yangu ya Gumzo, sasa
mashabiki wamekuwa wakinisumbua kuwa wanakitaka, nikaona kama wanakitaka
basi ngoja nitoe wimbo mzima, kama unavyojua mimi na majuto siyo
waimbaji ila tumeimba kwajili ya movie, lakini kwa sababu wanaitaka
naona bora tuwape ili wafurahi, pia kutokana na mashabiki kuona
wanaitaji wimbo wa Gumzo, wiki hii au ijayo tutafanya video yake ,kwaiyo
wadau wakae mkao wa kula' Alisema Nisha.

0 Comments