Muigizaji ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki, Zuena Mohammed ‘Shilole’
MUIGIZAJI Zuena Mohammed ‘Shilole’
amegandwa na madai ya utapeli kufuatia jamaa mmoja aitwaye Samir
kuibuka na kudai kuwa, walimpa shilingi laki mbili ili awakodishie
madansa kwa ajili ya video yao lakini mpaka sasa anachenga.
Samir alisema: “Shilole aliomba kiasi hicho cha fedha, meneja
wangu akamtumia lakini baada ya hapo ahadi zikawa nyingi na simu akawa
hapokei, sasa kama siyo utapeli ni nini?”
Akijibu tuhuma hizo, Shilole alisema kwa sasa yeye ana uwezo kifedha
hivyo hawezi kudhulumu kiasi hicho kidogo cha pesa ila wao
wanapowahitaji wacheza shoo wake wakarekodi, yeye anakuwa yuko bize
nao.”
0 Comments