
Mamlaka
ya Chakula na Dawa kanda ya kaskazini imekamata na kuteketeza
shehena ya vyakula madawa na vinywaji vyenye madhara kwa
wananchi vilivyokuwa vinaendelea kutumika katika maeneo mbalimbali
ya kanda hiyo na imewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa
kukabiliana na tatizo hilo.
Mkurugenzi wa TFDA kanda ya kaskazini Bw,Damasi Matiko
amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na mamlaka hiyo tatizo
bado ni kubwa na ushirikiano wa wananchi unahitajika ukiwemo wa
kuwa makini katika matumizi ya bidhaa zote na kutoa taarifa
pindi wanapobaini mapungufu.
Afisa afya wa manispaa ya jiji la Arusha Bw Leny Sumari
amesema madhara ya matumizi ya bidhaa bandia ama zilizopita muda
wake ni makubwa zaidi kwa watoto na ameikata jamii kuwa makini
kwa kuchunguza zaidi bidhaaa zinauzwa kwa bei rahisi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwemo Bw, Julius Moses
,Peter Ngusa , na Simion Mollel pamoja na kuipongeza TFDA kwa
jitihada wanazofanya wamesema bado ziko taasisi nyingine za
serikali ambazo hazijatimiza wajibu wake ipasavyo.
0 Comments