Mwenyekiti
wa Club ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
ndoto yake ni kuwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu hapa
nchini ikiwa ni pamoja na kuwa Rais kwani uwezo wa kuwaongoza
watanzania anao.
Akizungumza
na Mpekuzi, msanii huyo amesema kuwa kitendo cha kuchaguliwa
kuwa katibu kata ya Bwawani, Kinondoni jijini Dar es Salaam
kupitia chama cha Mapinduzi CCM, ni mwanzo mzuri wa kuelekea
kutimiza malengo yake.
“Hakuna
aliyezaliwa akitambua kuwa siku moja anaweza kuwa miongoni mwa
viongozi wakubwa katika nchi hii, lakini dalili za kuwa huko
huja kutokana na kuwa na malengo mazuri na kujitambua kama
unaweza kuwaongoza watu wengine,” alisema Steve Nyerere.
Msanii
huyo alisema hakuna kiongozi anayeweza kushika nyadhifa za juu
bila kuanzia chini kama alivyoanza yeye na ndio maana wabunge
wengi huwa wanaanzia chini na taratibu wanakuwa wanapanda
ngazi kwa lengo la kuona uwezo wao wa kuongoza.
0 Comments