Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika jana Julai 17, 2014 kuelezea msimamo wa
jukwaa la katiba juu ya mwenendo uliopita wa bunge hilo.
Kiongozi
wa Shule Kuu ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba
alisisitiza suala la wanasiasa kurudi bungeni na kuhakikisha katiba mpya
inapatikana.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

Wajumbe wa jukwaa la katiba wakisisitiza jambo.




Ushauri
Umetolewa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuwa na Mtazamo mpya
utakaoiletea nchi maslahi pindi watakaporudi bungeni katika mchakato
wakutafuta katiba mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Hata hivyo
kundi la Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) limezidi kushauri wakirudi
bungeni na kuendelea na majadiliano kwa msingi wa rasimu ya katiba.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam jana Julai 17, 2014 na mwenyekiti wa
Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba ambapo ameeleza kwamba wabunge
wanatakiwa kuachana na mtazamo wa kisiasa pamoja na lugha zisizo na staa
kwenye bunge hilo kwani wanatakiwa kuzingatia uzalendo kwanza.
Aidha Bw.
Kibamba amesema kwamba licha ya muda kuwa mfupi kuelekea katika uchaguzi
wa mwaka 2015 wao wanapendekeza juhudi zaidi zifanyike ili kukamilisha
upatikanaji wa katiba hiyo.
Naye Kiongozi
wa shule kuu ya Sheria nchini Kenya Profesa Patrick Lumumba amewasihi
wanasiasa wa nchini kuhakikisha katiba inapatikana kutokana na matakwa
ya wananchi kwani nchini jirani zimekuwa zikiiga mambo mengi kutoka
huku.Bunge Maalum la katiba linatajiwa kuanza tena Agosti 5, 2014 mwaka huu.
0 Comments