Ndikumana
ambaye kwa sasa anaichezea Vital’o ya Bujumbura, Burundi ameweka wazi
kwamba binti huyo, Irene Uwoya ambaye ni mkewe ni shabiki wa Jangwani na
amekua akimshawishi kila mara kwamba atue Jangwani ili awe naye karibu
zaidi kwani hana mpango wa kuondoka Dar es Salaam kwenye kazi zake za
filamu.
Mchezaji
huyo amekiri kushawishiwa mara nyingi lakini alisema hawezi kujipeleka
Yanga mpaka timu hiyo itakapomfuata, kama hiyo haitoshi aliongeza kwamba
anaogopa kuishi Dar es Salaam kutokana na mambo ya ushirikina
yaliyomtokea alipoanza maisha na mkewe ambaye ameshangaa watu wanaozusha
kwamba wameachana.
“Ananitaka
nije kucheza Tanzania alikuwa ananiambia nije Yanga, unajua anaipenda
sana Yanga lakini nikamwambia mimi ni mchezaji ninayejiamini siwezi kuja
kuomba Yanga wanisajili acha waje wao tuzungumze, yuko tayari kufanya
hata ushawishi kwa wadau,” anasisitiza Ndikumana ambaye awali alikuwa akiichezea APOP Kinyras Peyias ya Cyprus.
Ndikumana alisema kilichomtoa Cyprus na kuja Burundi pamoja na uhusiano wake na Uwoya.
“Kweli
nilikuwa Cyprus kama unavyosema lakini kikubwa ambacho kilinirudisha
Tanzania ni pale mke wangu alipokaribia kujifungua, niliporudi tu baada
ya muda nikaanza kuumwa sana na hivyo kushindwa kurudi Cyprus,” anasimulia.
“Tatizo
hilo naweza kusema ni mambo yetu ya Kiswahili na ni huko Tanzania ndiyo
kulikuwa chanzo, kuna vitu vilikuwa vinanitokea mwilini kiasi kwamba
nilikuwa najikuna sana mwili mzima, hospitali nilikwenda na kupima
vipimo vyote hakukuonekana kitu, kuna wakati wakaniambia ni fangasi.
“Nikaona
hapana bora nigeukie upande wa pili wa tiba asilia, nako hali haikuwa
rahisi nilizidi kuteseka ilifikia hatua najikuna mpaka vidonda vinatoka
miguuni nikaona sasa na vidonda hivi nitarudije Cyprus bora nitibiwe
kwanza kabla ya kuondoka.
“Ukweli
ni kwamba nilizunguka sana kwa wataalamu mbalimbali kiu yangu ilikuwa
ni kuhakikisha nakuwa sawa, nakumbuka mwanzoni kama ndani ya miezi
miwili nilitumia hadi Sh6milioni kusaka tiba lakini bado ikashindikana,
nilikuwa nataka kuhakikisha napona haraka ili niwahi kurudi kazini.
“Nilizunguka
sana nakumbuka baada ya kuona Tanzania ni vigumu nikaondoka na kuja
hapa Rwanda nako nilitibiwa hali haikuwa sawa, nikaenda DR Congo kidogo
nikapata nafuu lakini baadaye kuna mtalaamu mmoja akanisaidia tena kwa
kiasi kidogo maradhi yakapungua.
“Kuna
mtu namjua kwamba alikuwa akifanya haya yote, hili nililiamini baada ya
kumrudia Mungu, ukiacha ya Mungu pia hata hao wataalamu karibu wote
nilipokuwa napita walikuwa wakimtaja sioni kama walikuwa wanadanganya
kwani ni watu tofauti wote wamemtaja mtu mmoja, namuachia Mungu na
nashukuru sasa nimeanza kurudi katika hali yangu.
“Baada
ya misukosuko yote hiyo Baba yangu (Ndikumana Kitenge) kule nyumbani
ana timu yake ndogo ya vijana, nikawa natumia muda huo kumsaidia
majukumu ya kuwafundisha vijana na hapohapo na mimi nafanya mazoezi,
nilipoona hali imeimarika nikaenda Vital’O kuwaomba nifanye nao kazi
wakakubali na nashukuru walinielewa na kuniamini sasa nipo nao kwa muda.“Sijasaini mkataba na Vital’O unajua kuna wakati nafanya mazoezi kuna timu za Ulaya zilikuwa zinataka kunifuata nikaona niende Vital’O ili nijiweke sawa endapo watakuja wanikute katika hali nzuri lakini hao jamaa walivutiwa na mimi wakati nacheza kama beki na sasa hapa natumika kama kiungo mkabaji sijajua kama wakija watanikubali.”
Alikutana wapi na Uwoya?
“Unajua Irene nilimpenda kupitia filamu nilipomuona nikataka siku moja nikutane naye, nashukuru Mungu kuna siku wakati nataka kwenda Kigoma katika harusi ya dada yangu nilipitia Dar es Salaam nikakutana naye pale uwanja wa ndege.
“Sijabadili dini, ni kweli kwamba tulifunga ndoa ya kanisani lakini sikubadili dini nilitajwa kwa jina la Hamad Ndikumana, tulikubaliana na mke wangu tufunge ndoa mbili ya Kikristo na Kiislamu ikatangulia ile hii nyingine tukasema tutaifunga baadaye lakini muda ukawa mdogo ila tutaifunga hakuna shida.
Ni kweli wameachana na Uwoya?
“Kwanza nashangaa hao wanaodai nimeachana na mke wangu wanajua nani amempa talaka mwenzake? Sijaachana na Uwoya, yule ni mke wangu isipokuwa kwa sasa ni kama tumetengana na huko si kuachana labda watu wanachanganya mambo.
“Kuna mambo tulishindwa kukubaliana, alikuwa hataki kuja kuishi na mimi kule Cyprus, alikuwa anataka tuishi Tanzania tu, sasa mimi kazi yangu ni soka siwezi kuacha kazi ili nirudi Tanzania niishi na familia yangu bila ya kuwa na kazi hilo lilitufanya tutengane kidogo.
“Achana na mtoto nipo na maelewano mazuri na Uwoya hadi sasa tunawasiliana ngoja nikuthibitishie (Anainua simu na kumpigia lakini haipokelewi) nadhani atakuwa katika kazi zake, yupo safarini Afrika Kusini amekwenda kurekodi filamu na hata Krish ni mwanangu kila ninapotaka kumuona namuona bila shida.
“Sasa ana miaka mitatu na tumeshamwanzisha shule, anasoma (ananionyesha video fupi Krish aliyorekodiwa akihesabu namba kwa Kiingereza) nadhani sasa utaniamini unajua watu hawajui mimi na Irene ni wapenzi na tunaonana kila tunapopata nafasi.
“Hayo ni maneno ya watu tu, unajua Tanzania maneno ni mengi sana, kweli kuna wakati yanasemwa mengi sana ninaposikia nakutana na mwenzangu namuuliza anakataa lakini ukiacha kukataa kwake hata mimi nimeshindwa kuthibitisha hayo madai kwa hiyo nayaacha maisha yanaendelea.
“Kila kitu kina muda wake bado naamini siku moja nitarudi kuwa karibu na familia yangu, kwa sasa acha kwanza kila mmoja afanye yake ya kikazi, baadaye tutatulia na kuwa pamoja, watu waache kutugombanisha,”anasisitiza.
Tupe maoni yako hapo Chin