
Waziri
wa Ujenzi John Magufuli amesema Serikali inatarajia kuongeza kivuko
kingine cha kuvusha watu Kigamboni ambacho kitagharimu shilingi bilioni
3.7 wakati ujenzi wa daraja ukiendelea.
Anasema daraja linalojengwa sasa hivi litakamilika June 2015 badala
ya July kama ilivyokua imefahamika mwanzoni ambapo tayari Mkandarasi
ameshalipwa shilingi Bilioni 117 kati ya 214 za kukamilisha mradi wote
limeandika gazeti la Tanzania Daima.

Nalo
gazeti la HabariLEO August 9 2014 limeandika >> Magufuli abana
wenye magari Kigamboni, ataka wasisumbue abiria wa Pantoni asubuhi na
jioni, wenye haraka watakiwa kuzunguka Kongowe – Mbagala, ni agizo la
muda mfupi baada ya kivuko kilichopo kuzidiwa.
0 Comments