
STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha', Jumanne iliyopita alijikuta akizua taharuki kufuatia kuegesha gari lake nje ya Hekalu la Freemason lililopo nyuma ya Hyatt Regency Dar es Salaam The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam
Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Taharuki
hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka
kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka
kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila
anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo.
Chanzo chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi huonekana wakiingia na kutoka.

“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.
Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye.