Mwana
Diplomasia kutoka Ghana ambaye pia ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa
Mataifa (UN) Kofi Annan amesema ugonjwa wa Ebola ni wa ‘maskini’ na sio
matajiri.
Annan
amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha CNN ambapo
amezungumzia sababu kadhaa zinazopelekea mapambano ya dhidi ya Ebola
kuchukua muda mrefu huku maelfu ya watu wakipoteza maisha.
Katibu
Mkuu huyo mstaafu amesema Ebola ni ugonjwa wa maskini kwa kuwa tangu
ugundulike ni takribani miaka 40 imepita, ambapo kwa nchi tajiri
ingewezekana kufanyika tafiti ambazo zingesaidia kupata ufumbuzi wa tiba
ya ugonjwa huo, kitu ambacho nchi maskini za Afrika hazina uwezo wa
kuwekeza kwenye tafiti hizo.
Aidha,
Annan ameonekana kuvunjwa moyo na jitihada zinazofanywa na mataifa
makubwa ikiwemo Marekani kutangaza utaratibu mwisho wa wiki iliyopita wa
kuwaweka karantini wauguzi na madaktari waliotoka Afrika Magharibi kwa
siku 21, kitu ambacho kinarudisha nyuma ari ya wahudumu hao kujitolea
kusaidia wagonjwa kwenye nchi zilizoathirika na Ebola.
Amesema
njia pekee ya kuimaliza Ebola ni kufanya jitihada na mapambano ya
pamoja katika kuzisaidia nchi za Afrika Magharibi na sio kwingineko, na
kuongeza kuwa Afrika inachohitaji ni msaada wa vifaa, madawa na wauguzi
ili kupambana na Ebola.
Mpaka
sasa Liberia, Guinea na Sierra Leone zimetajwa kuathiriwa zaidi na
Ebola,huku takwimu zikionesha zaidi ya watu 4,900 wamefariki na wngine
zaidi ya 10,000 kupatwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
0 Comments