
Makamu wa rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ambaye aliwahi kufanya
kazi pamoja na Dk. William Shija kama katibu mkuu wa wizara ya Sayansi,
Teknolojia na elimu ya juu kwa miaka 10 amesema kuwa marehemu Dk.
William Shija alikuwa mchapakazi hodari, mwenye bidii, mwadilifu na
aliyependa watu, hivyo kifo chake ni pigo kubwa siyo tu kwa watanzania
bali katika jumuiya ya kimataifa ambako amehudumu kama mtu wa kwanza
mweusi kuwa katibu mkuu wa mabunge ya jumuiya ya madola tangu kuanzishwa
kwa jumuiya hiyo mwaka 1911.
Kwa upande wake spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mh. Anne Makinda amesema upinzani sio uadui, na kuwataka wanasiasa kuiga
mfano wa maisha ya Dk. William Shija ya uadilifu na kutojilimbikizia
mali huku mwakilishi wa bunge la Kenya Seneta Moses Watangula akisema
kwamba umoja wa mabunge ya jumuiya ya madola umeondokewa na mtu shujaa
ambaye alisimama imara kupinga kila aina ya ubaguzi uliokuwa ukifanywa
na wazungu dhidi ya waafrika.
Mtoto wa marehemu Dk. Shija, Anna- Claire Shija amesema familia
hiyo daima itaendelea kumuenzi marehemu baba yao kwa matendo mema,
ambapo Padri Revocatus Makonge wa parokia ya Nyampande akihubiri katika
ibada ya misa yamazishi iliyoongozwa na askofu wa kanisa katoliki jimbo
la Bunda ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa jimbo la Geita mhashamu
Renatus Nkwande walikuwa na haya ya kusema marehemu Dk. William Shija
ambaye alizaliwa mwaka 1947 wilayani Sengerema ameacha mjane na watoto
watano.
0 Comments