
Shamsa Ford
Katika maisha ya kawaida ya Binadamu yoyote kuna vitu unaweza kuviona
moja kwa moja hata unapoishi nae lakini kuna vingine ni mpaka akueleze
mwenyewe,Leo
Shamsa Ford kutoka kiwanda cha Filamu
Tanzania kaamua kuchukua time yake kutueleza vingine tusivyojua kuhusu yeye kwenye upande hasi wake.
Kwenye akaunti yake ya
Instagram
ameweka picha yake kisha akaandika haya>>Morning my PEOPLE..HIZI
NDO MY NEGATIVE SIDES ..(1) nina wivu kupitiliza kwa mtu ambae nampenda
ingawa sioneshi (2)nina kaukorofi nikiudhiwa (3) nina hasira sana (4) ni
mtu ambae nikiamua langu nimeamua.
Hapa anaendelea (5) mm ni msiri mnooooo (6)ni mtu ambae ni mzito
kusema shida yangu niko radhi nife nayo kimiya kimiya (7)ni mgumu
kusamehe (8)mtu anaweza kunikosea na nikakaa kimiya nisimuulize na
nisimuoneshe tofauti yoyote (9) ni mwepesi kuamini watu (10) ni mbishi
kidogo (11) ni mtu ambae nafwata sana moyo wangu kuliko akili yangu (12)
ni mtu ambae nikiamua langu lazima nilitimize.
Zingine alizoandika ni (13) ni mtu ambae napenda sana kusema ukweli
mwisho wa siku inaniongezea maadui (14) huwa sitabiliki naweza nikawa
mpole pia naweza kuwa mkorofi (15)napenda kudekezwa (16) ni mtu wa
kupuuzia vitu (17)muda mwingine najiamini kupitiliza (18) nikimpenda mtu
namuonesha na nikimchukia mtu lazima ajue coz sijui kupretend (19) huwa
sikubali kushindwa (20)nikiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu
ambae nampenda huwa nasahau kabisaa marafiki (21) … ZINGINE NITAMALIZIA
BAADAE ZIMEBAKI NEGATIVE SIDES ZANGU 30
0 Comments