Pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini NCCR Mohamed Tibanyendera akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Picha: Karoli Visenti.
SIKU moja kupita baada ya Makamu mwenyekiti wa chama cha NCCR-mageuzi, Reticia Mosore pamoja Katibu Mkuu wa chama hicho John Mwambabe kuibuka na kumtuhumu Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia kukiua chama chao kwa kile wanachodai kuwa wamepewa majimbo machache ya uchaguzi,Chama hicho kimeibuka na kusema wanasikitika na viongozi hao kubadilika dakika hizi za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu kwani hatua zote za ugawaji wa majimbo hayo viongozi hao walishiriki kwenye hatua zote.

Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza la
wadhamini NCCR Mohamed Tibanyendera amejibu malalamiko hayo kwa kusema
Chama hicho kimesikitishwa na kauli za viongozi hao kipindi hiki cha
mwisho kwani maamuzi yote yaliyofikiwa na UKAWA yalifuata kanuni zote na
kwamba hata ofisi ya Katibu mkuu huyo ndio ilikuwa inahusika katika
majimbo hayo
“Sisi
NCCR tunashangaa kwa kauli za Katibu wetu pamoja na Makamu mwenyekiti
kwani kipindi majimbo yagawiwa kwenye vyama, Ofisi ya Katibu ilikuwepo
na ndio ilikuwa inapanga majimbo hayo.
"Ugawaji
wa majimbo ulizingatia ushindani wa kisiasa pamoja na nguvu ya eneo
husika. Wote kwa pamoja tulikubaliana na hali hiyo, sasa tunashangaa leo
wanakuja kubadilika” amesema Tibanyendera
Amesema Majimbo 22 walioyopata NCCR kwa upande wa Ukawa ni mengi sana ukizingatia na miaka ya nyuma
“Jamani
NCCR tumekaa zaidi ya miaka 10 bila hata kuwa na mbunge hata mmoja,
2010 tukapata wabunge 4 tu wakuchagulia,sasa leo kupitia ukawa,NCCR
imesimamisha wabunge 22 kupitia majimbo tofauti nchini maana yake ni
zaidi ya mara 5 ya wabunge tuliopata sasa, huku wabunge wetu 4 waliopo
wanaendelea kugombania” amesema
Tibanyendera
ameongeza kuwa madai wanayotoa yalitakiwa kutolewa kwenye vikao halali
vya chama hicho kwa mujibu wa katiba ya chama.
Tibanyendera
amedai kuwa viongozi hao walikuwepo kwenye kikao kikuu kilichofanyika
tarehe 16 mwezi huu, na suala hilo wanalodai hawakulizungumia kwenye
kikao hicho lakini wanashangaa leo kuibuka mbele ya vyombo vya Habari
na kutoa lawama kwa mwenyekiti .
Aidha,Tibanyendera
amewataka Wanachama vya Vyama vinavyounda UKAWA ambavyo ni Chadema,Cuf
na NLD kupuuza madai ya viongozi hao na kuyachukulia ni watu binafsi na
sio ya chama ,akidai kuwa NCCR itaendelea kuwa sehemu ya UKAWA na
kitakuwa chama cha mwisho kujitoa ukawa.
Amewataka
watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya Octoba 25 mwaka huu na
kumchagua mgombea wa Urais kupitia umoja huo Edward Lowassa pamoja na
wabunge na madiwani wanaounda Ukawa.
Mpekuzi blog
0 Comments