Mwanamuziki mkongwe wa Congo, Pascal Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa katika hospitali ya nchini ubelgiji.
Kwa mujibu wa mwanae Charles Tabu, Baba yake amefariki kwa uginjwa wa Kiharusi na kisukari.
Naye Nyboma Mwanandido,
mwanamiziki mwenzake aishie Pars Ufaransa, amethibitisha kutokea kwa kifo cha
Tabuley.
Tabuley alikuwa mgonjwa
mahututi katika hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa na Kiharusi alichokipata
mwaka 2008.
Kiharusi, yani Stroke
kilimfanya awe kwenye kiti cha walemavu tangu wakati huo.
Pamoja na muziki Tbuley
aliwaki kuteuliwa kuwa waziri nchini Congo na rais Laurent Kabila mwaka 1997 na
baadae pia kuwa mbunge.
Miaka ya mwishoni mwa uhai
wake alikuwa akiishi Paris, Ufaransa kabla ya hivi karibuni kupelekwa Ubelgiji
kwa matibabu maalumu.
Katika mika yake 46 ya
muziki, Tabuley ameshaandika zaidi ya nyimbo 3,000 na kuuza maelfu ya nyimbo.
Tabuley, aliyezaliwa
November 13, 1940, alikuwa kiongozi wa kundi la Orchestre Afrisa International
na mmoja wa wasanii wakubwa katika bara la Afrika katika uimbaji na utunzi wa
nyimbo.
Akiwa na mpiga gitaa
hodari Dkt Nico Kasanda, Marehemu Tabu Ley alikuwa mwanzilishi wa mtindo wa
Soukous, na kuufanya ukubalike kimataifa kwa kuchanganya midundo ya Cuba na
Rhumba la Latin Amerika.
0 Comments