‘VIDEO
queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka kuwa
aliyempa mzigo wa unga na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa amevalia kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua. Taarifa
za uhakika kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na
kudhibiti madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa
mwanadada huyo alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu
ambaye hamjui aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea. “Alidai
kuwa kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale
ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa
kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka
kusikojulika,” kilisema chanzo. Kwa
upande wake, Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya
nchini, Godfrey Nzowa alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa
Masogange aliwaeleza polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni
mtu aliyekuwa amevalia kininja.
0 Comments