
Diamond alimzawadia mzee Gurumo gari mpya mwaka jana wakati wa uzinduzi wa video yake ya ‘Number 1’.
Platnumz amesema meneja wake Babu Tale alimpa taarifa hiyo njema ya kuandikiwa wimbo na Gurumo lakini kwa bahati mbaya mzee Gurumo alifariki kabla hajamkabidhi wimbo huo.
“Juzi kampigia simu Tale akamwambia kuna nyimbo nimemtengenezea Diamond kwasababu kwa alichonifanyia mimi nimeshukuru sana cha kumlipa mimi sina lakini nimemuandikia nyimbo” amesema Platnumz.
“so alikuwa anamwambia Tale kama ameniandikia nyimbo, so angependa anipatie nikamwambia sawa. Kama siku tatu hivi nyuma, jana ndio nasikia taarifa hizi so najiona kama nimechanganyikiwa hivi.”
Platnumz ameongeza kuwa mara ya mwisho kuonana na Gurumo ilikuwa ni takribani wiki tatu zilizopita baada ya mwimbaji huyo mkongwe kumsurprise kwa kuhudhuria katika show aliyokuwa anatumbuiza Diamond kwa lengo la kutaka kumwona na kumshukuru kwa zawadi ya gari aliyompatia.
“Mara ya mwisho kukutna naye nilikuwa nafanya show Coco akaja maskini ya Mungu mpaka kwenye show…kama wiki moja nyuma kama sikosei au wiki mbili.
Akaja
akasema nimekuja hapa kukuona, alipenyapenya hadi akaweza kufika
pale…nilivyomuona anakuja ilibidi pale nikatishe show nikamsalimia
kidogo halafu nikaendelea na show, halafu baadae nikawa niko nae
backstage na nini nikazungumza nae.So akasema nimekuja kukushukuru sana
sana sana, akasema ningependa uje nyumbani nikamwambia sawa.”Amesema
Diamond.
Mwili wa marehemu mzee Gurumo umepelekwa kijijini kwake
Masaki, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kwaajili ya mazishi
yanayofanyika leo.
0 Comments