Makubwa! Kaka mkubwa kunako gemu la
filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ amefunguka kuwa
hana mpango wa kumuoa mwanadada Chuchu Hans kama inavyodaiwa na baadhi
ya watu. Akijibu swali aliloulizwa na wanahabari
wetu hivi karibuni, kuhusiana na kudaiwa kuwa baada ya mpenzi wake huyo
kupewa talaka ana mpango wa kufunga naye ndoa kama ilivyokuwa inadaiwa
ambapo alikataa katakata suala la yeye kufunga ndoa na Chuchu. “Sina mpango wa kuoa ndugu yangu, hayo
ni maneno ya watu ambayo yapo tu mitaani ila kwa sasa niko njiani naenda
gym baadaye nitakutafuta tuongee.” alisema Ray. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa
muigizaji huyo kufunguka kuhusiana na suala la ndoa na swali linakuja,
je, Chuchu anafahamu kuwa anachezewa tu? Jibu analo mwenyewe moyoni
mwake.
0 Comments