
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Palycarp Kardinali
Akizungumza katika sikukuu ya mapadri na kubariki
mafuta ya krisma katika Kanisa la Mtakatifu. Joseph, Dar es Salaam,
Pengo alisema ndoa za mkataba zinachangia kwa kiasi kikubwa wanandoa
kutokuwa waaminifu na kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinazaa
familia ambazo hazina maadili.
“Kuna wanandoa wanaona kukaa na mwenza wake kwa
muda wote ni jambo ambalo halikubaliki, wanajiingiza katika ndoa za
mkataba ili waweze kufanya matendo mengine ambayo hayampendezi Mungu na
hapo ndipo wanajenga familia isiyokuwa na maadili,” alisema.
Kuhusu ushoga, Pengo alisema: “Hatuwezi kuwa na
familia imara kama hatutakemea mazingira haya ya ndoa za jinsi moja na
hatuwezi kuzungumzia uhai wa kuwa na familia bora wakati kuna kikwazo
ambacho hakiendani na maadili ya dini zote.”
Kardinali Pengo pia aliwaonya mapadri wanaotumia
fedha za kanisa kwa masilahi binafsi akiwataka kuacha tabia hiyo mara
moja. Alionya kwamba endapo watabainika, kanisa halitatoa fedha kulipa
faini au fidia itakayotokana na uzembe huo.
Aliwashukuru waumini wa Dar es Salaam kwa kumpatia
zawadi ya Sh43 milioni wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya uaskofu na
kuahidi kuzitumia katika ujenzi wa Shule ya Msingi Kisiwani iliyopo
Mafia.
0 Comments