January Makamba.
1. ‘Kama
tunataka kuuvunja muungano wetu ndani ya mwaka mmoja au miwili….
tuingie kwenye serikali tatu, itakua ni janga kubwa sana kuiua hii lulu’
2. ‘Nchi
nyingi za Afrika zimetengenezwa na mipaka ya Wakoloni, sisi Waafrika
ndio tumetengeneza kitu chetu wenyewe na tukakipa jina wenyewe na
kukiita Tanzania, kama tunataka ulimwengu utucheke… tuue kitu chetu
wenyewe’
3. ‘Nimeisoma
rasimu, ukitazama kitu cha kwanza baada ya sisi kupitisha serikali tatu
tunakwenda kwenye mpito ambako kwenye masharti ya mpito ibara ya 269
kifungu cha kwanza kinaeleza mambo yatakayofanyika kwenye kipindi cha
mpito, ni kugawana mali, madeni na watumishi’
4. ‘Kitendo cha kugawana mali, kugawana madeni, kugawana Watumishi…. kitendo cha kugawana hivyo vyote ni kitendo cha utengano’
5. ‘Kwenye
mgawanyo huohuo wa kugawana mali hata kabla hatujaanza kwenye serikali
hii ya shirikisho ndio itakua mwisho hapohapo, tukipitisha hii kitu..
mwaka mzima miaka miwili tutahangaika na mjadala wa kugawana’
6.‘Sisi
wengine tumo humu baadhi yetu tutakuja kuongoza nchi hii, hatutaki kuja
kuongoza taifa ambalo tunahangaika na taratibu za kugawana mali,
taratibu za utengano’
7. ‘Viongozi
tunaokuja tunataka kulijenga taifa kubwa na lenye nguvu zaidi na
tutalijenga kama tutakua na umoja, hatutapenda kuhudhuria vikao vya
kugawana mali, tunazo kazi nyingi za kimaendeleo… watu wetu wana
mahitaji mengi’
8. ‘Tumetumia
muda mrefu sana hapa kubishana kuhusu takwimu, ziko namna mbili za
kujua utashi wa watu kwenye mambo makubwa, ya kwanza ni kupiga kura ya
maoni kuwauliza wanataka nini… hatujalifanya bado, la pili ni kutazama
matokeo ya uchaguzi na sera za vyama kuangalia chama gani kimeshinda
hivyo kujua ni sera gani inayotakiwa’
0 Comments