Ni msanii mwenye ups and downs nyingi
sana , kama unatafuta role model hapa bongo basi muite Shilole. Alianzia
kwenye movie lakini kabla ya movie alishawahi kuuza chakula na biashara
mbali mbali in order to survive.
Shilole katika pitapita zake kwa bahati
mbaya alijikuta akilazishwa mapenzi wakati akiwa na umri mdogo sana,
msanii huyo akiwa na miaka 14 tu alijikuta akiwa na mimba . “nilipata
mimba nikiwa mdogo sana yani hata maziwa ndio yanaanza sipendi kitu hiki
kimtokee msichana mwengine kwa kweli na pia kwa wale wanaume wenye
tamaa plz wanapoteza future za watu” alisema shilole.
Baada yakupata mtoto wake huyo,
aliangaika nae na baadae alijikuta akiolewa na mtu mwingine na kuweza
kupata mtoto wake wa pili akiwa na umri wa 18 na mwisho wa siku alitoka
ndani ya ndoa na kuhamia Dar na kuanza maisha upya.

0 Comments