Anaweza kuingia kwenye stori za siku tena kubwa na si ukubwa wa kuoa tu ni ukubwa wa kufunga ndoa tena ikiwa ya kimya kimya bila baadhi ya mastar wenzake kuhusika na harusi hiyo ambayo wengi wamesema ilikua kama ya ghafla.
Miaka kadhaa nyuma D.Knob aliwahi kufunga ndoa ya namna hii ambayo
kwa maelezo yake alisema kuwa harusi yake hawakuzidi watu 15 kuanzia
Kanisani mpaka sehemu waliyoamua kukaa na kupata vinywaji kadhaa.
Amini Mwinyi Mkuu kutoka THT amefata nyanyo za D.Knob na wasanii
kadhaa ambao waliwahi kufuga ndoa za kimya kimya kwa Amini ndoa yake
ilifungwa Msikiti wa Ibazi uliopo Manzese baada ya swala ya saa 2
usiku, idadi ya watu walioshuhudia ndoa hiyo hawakuzidi watu 20 na hiyo
ni jumla ya wazazi pamoja na wasindikizaji.
Amini kafunga ndoa na msichana anaeitwa Farida Bashir au Namcy Vana
ambaye sauti yake imesikika kwenye wimbo wa Kantangaze uliotoka miezi
kadhaa iliyopita,Miaka kadhaa nyuma Amini amewahi kuripotiwa kuwa na
uhusiano na msanii mwezake Linah.

0 Comments