Mwanamke
Meriam Ibrahim aliyeachiwa huru juzi baada ya kuhukumiwa kifo kwa kosa
la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu amekamatwa
tena akiwa na mumewe pamoja na watoto wawili katika uwanja wa ndege
mjini Khartoum, Sudan.
Meriam
amekamatwa na watu takribani 40 waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia
ikiwa ni masaa machache baada ya kuachiwa huru kutokana na uamuzi wa
mahakama ya rufaa.
Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuasi dini
Inadaiwa kuwa Meriam aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
0 Comments