Advertisement

Responsive Advertisement

BREAKING NEWS: WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NA PEMBE ZA NDOVU WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR


VIJANA wawili Dominick Kombe (36) na Hebert Macheka (30) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kesi ya kukamatwa na vipande 28 vya pembe za ndovu vyenye thamani ya shilingi milioni 275.
Watuhumiwa hao walikamatwa Juni 5 mwaka huu eneo la Tabata, Kisukulu jijini Dar wakiwa na nyara hizo za serikali ambazo hazikuwa na kibali chochote kinyume na sheria.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Waliyarwanda Lema chini ya mwendesha mashitaka wa serikali Ofmedy Msenga, imeahirishwa mpaka Julai 9 mwaka huu itakaposikilizwa tena baada ya watuhumiwa kutotimiza vigezo vya dhamana.
(Habari: Haruni Sanchawa / GPL)

Post a Comment

0 Comments