WATU
watano wamepoteza maisha baada ya shambulio lililotokea usiku wa
kuamkia leo katika kijiji cha Pandanguo huko Witu wilayani Lamu nchini
Kenya kilometa 30 kutoka Mpeketoni yalipotokea mauaji ya watu zaidi ya
60 wiki iliyopita.
Polisi wamesema kuwa waliouawa ni kutoka jamii mbalimbali.
Mkuu wa
Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo amesema kuwa washambuliaji walivamia
kijiji cha Pandanguo na kuua takribani watu watano.
"Bado tunawasaka waliohusika na shambulio hili, habari zaidi zitatolewa baadaye," alisema Kimaiyo.
0 Comments