Eneo jipya la kutafuta ndege ya Malaysia iliyopotea limetangazwa na
serikali ya Australia baada ya taarifa mpya za Satellite kutolewa.
Kwa mujibu wa waziri mkuu Warren Truss, zoezi la utafutaji wa ndege
hiyo sasa litahamia Kusini kuegemea eneo la kilomita 1,800 kutoka Pwani
ya Magharibi ya Australia.

Ndege ya MH370 ilipotea wakati wa safari yake kutokea Kuala Lumpur
kwenda Beijing Machi 8 mwaka huu ikiwa na abiria 239 ndani yake.
0 Comments