Kesi dhidi ya mshukiwa mmoja anyetuhumiwa kumbaka msichana mmoja katika eneo la Bumala Magharibi mwa Kenya imeahirishwa.
Mshukiwa mmoja kati ya sita wanaodaiwa kumbaka
na kumtupa katika shimo msichana huyo kwa jina Liz, alifikishwa
kizimbani na kufunguliwa mashtaka ya kumbaka na kujaribu kumuua msichana
huyo, katika kisa ambacho kimezua hasira na hamasa miongoni mwa wakenya
wa tabaka zote
Kinyume na kesi zingine, kesi hii
iliendeshwa faraghani huku mawakili wanaowakilisha pande husika na
maafisa wa mahakama ndio walioruhusiwa kuwepo mahakamani.
Afisa kutoka ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu
aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni mkubwa pekee ambaye anapaswa
kuzungumzia suala hili, kutokana na uzito wake.
Mawakili wa mshichana huyo wamesema kuwa wao
waliamua kuomba kesi hiyo kuendeshwa faraghani ili kumlinda mhusika
ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18. Pia uamuzi huo ulichukuliwa ili
kuwapa wanaohusika Imani ya kutoogopa mtu yeyote.
Mwandishi wa BBC ambaye yuko mjini Busia Robert
Kiptoo, anasema kuwa kinyume na ilivyokuwa Jumatatu wakati mamia ya watu
waliandamana, leo hali ilikuwa shwari huku jamaa na marafiki tu ndio
waliofika mahakamani.
Liz alitoa ushahidi wake leo asubuhi na kisha
kuhojiwa nyakati za alasiri kuhusiana na tukio hilo ambalo lilimuacha
kama amelemazwa kabisa.
Washukiwa wengine watano bado wanasakwa na
polisi na duru zinasema kuwa wazazi wao wamepewa ilaani kuwawasilisha
washukiwa hao mahakamani.
Liz inadaiwa alibakwa na wavulana sita Juni
mwaka jana na kututwa katika shimo la choo, hali iliyosababishia
majeraha ambayo kwa sasa yamemlemaza.
Tangu wakati huo wanaharakati wa kijamii
wamekuwa wakishinikiza mkuu wa polisi nchini Kenya kuhakikisha kuwa
waliombaka Liz wamefikishwa mahakamani.
Hata hivyho sakata hiyo ilichukua mkondo tofauti
pale, ilipofichuliwa kuwa waliombaka waliachiliwa huru na polisi baada
ya kuadhibiwa kufyeka nyasi katika kituo kimoja cha polisi.
Kesi dhidi ya mshukiwa mmoja wa ubakaji wa msichana Liz na kumjeruhi vibaya nchini Kenya imeahirishwa hadi tarehe 8 mwezi Juni.
Kesi ya Liz ilisababisha ghadhabu sana sio Kenya tu bali duniani kote hasa kwa ambavyo polisi waliishughulikia.
Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayopinga dhuluma dhidi ya wanawake, uliongoza waandamanaji ambao
baadaye walikusanyika katika kituo cha mkuu wa jimbo, Isaiah Nakoru.

Liz alibakwa mwaka jana na kuachwa na majeraha mabaya mwilini mwake Walimkabidhi mkuu huyo nyaraka zilizotiwa saini kutaka Liz atendewe haki.
Waliotia saini nyaraka hizo wanamtaka mkuu wa
polisi kuwakamata washukiwa na kitendo hicho cha unyama dhidi ya Liz
ambao walimbaka na kisha kutupa mwili wake ndani ya shimo lenye urefu wa
futi 25 mjini humo.
Viongozi wa maandamano wanasema kuwa idadi kubwa
ya wasichana waliobakwa tangu kusikika kwa kisa cha Liz wamekuwa
wakienda kuwashitaki watuhumiwa kwa polisi.
Liz alibakwa na wanaume sita ambao walimuwacha
na majeraha mabaya kwenye mwili wake kiasi cha kulazwa hospitalini kwa
miezi kadhaa.
Mamake Liz alikuwa miongoni mwa waandamanaji.
0 Comments