Kamati
ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA imemfungulia mashataka
mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez kufuatia tukio la
kumng’ata beki wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini, wakati wa
mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kundi la nne ambapo The Azzuri
walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri.
ona video chini bofya read more..
Kamati
ya nidhamu imethibitisha kumfungulia mashtaka mshambuliaji huyo mwenye
umri wa miaka 26, baada ya kupata ripoti ya mchezo huo ambao ulichezwa
kwenye uwanja wa das Dunas, uliopo mjini Natal.
Hata
hivyo kamati hiyo imetoa nafasi kwa Luis Suarez, pamoja na shirikisho
la soka nchini Uruguay kuwasilisha utetezi wao kabla ya kuanza
kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Nafasi
kwa Suarez pamoja na shirikisho la soka nchini Uruguay kuwasilisha
vielelezo vya ushahidi wa kupinga suala hilo, imetolewa hadi saa kumi
na moja jioni kwa saa za nchini Brazil.
Tayari
kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uruguay Oscar Tabarez ameshajiondoa
kwenye ushahidi huo, baada ya kukiri hakuliona tukio hilo ambalo
lilijitokeza katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Tukio
la Suarez kumng’ata Chiellini lilitokea dakika kumi kabla ya mchezo wa
Italia na Uruguay haujamalizika, ambapo picha za televisheni
zilionyesha kwa kurudia rudia tukio hilo ambalo linadaiwa huenda
lilikuwa halali kwa mshambuliaji huyo wa klabu ya Liverpool kuonyeshwa
kadi nyekundu.
ANGALIA VIDEO YA TUKIO HILO HAPA CHINI

0 Comments