Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997,
Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri
wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad
Wilson Ngewe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.
Kabla
ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa
Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa
Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi
kavu na Majini Tanzania.
0 Comments