Makundi mawili hasim ya wasanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja yajulikanayo kama 'Wema Team' na 'Kajala Team' yanatarajiwa kuvunjwa kwani ndio yameonekana kuchochea bifu la wawili hao ambalo limekuwa likionekana kuisha na kuibuka tena....
Akizungumza
na mwanahabari wetu, Kajala amesema kuwa tatizo lao limekuwa
likichochewa na makundi hayo hasa wanapotangaza kusamaheana na
kuzika tofauti zao makundi hayo huibuka na kuanza kutukanana,
kitu ambacho huzusha tena hasira zao....
"Siyo
siri, tatizo letu linachangiwa na hizi team ambazo zipo kwa
ajili ya kuongeza matatizo.Tunafikiria kuyavunja kwani kwa sasa
yameonekana kutokuwa na faida zaidi ya kuzidisha hasira ambazo
tumekuwa tukizizika kila tunapotangaza kusameheana," alisema Kajala.
Msanii
huyo alisema hawaoni haja ya kuwa na makundi ambayo
hayawatakii mema kwani katika maisha kukosana kupo lakini pia
kusameheana ndo jambo la busara kwani hakuna aliyemkamilifu
hapa duniani.
0 Comments