VITUKO uswahilini! Mtoto wa mwenye umri umri wa mwaka mmoja
ambaye jina halikufahamika ameokolewa baada ya kudaiwa kutelekezwa kwa siku nzima na mama
yake mzazi, Mama Sofia.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Juni wikiendi iliyopita maeneo ya
Somanga-Magomeni, Dar ambapo kwa mujibu wa wasamaria wema waliomuona
mtoto huyo, alionekana majira ya asubuhi akirandaranda barabarani.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na mama yake.
Baada ya waandishi wa habari kufika eneo la tukio ambapo ilipata
maelezo kuwa mama wa mtoto huyo huwa na tabia ya kumwacha mwanaye mara
kwa mara mtaani bila kumjali.
OFM ilifikisha suala hilo kwa mjumbe wa mtaa huo ambaye alimtambua mtoto huyo mara moja kwa kuwa alikuwa akiishi naye nyumba moja hivyo alimpeleka kwa wazazi wake huku akiwapa onyo kali.

0 Comments