
Jeshi la polisi mkoa wa Mara linamshikilia kijana mmoja ambaye ni
mwanafunzi wa kidato cha 2 katika shule ya sekondari ya Kemoramba
wilayani Butiama, baada ya kutuhumiwa kumbaka mtoto wa kaka yeke mwenye
umri wa mwaka mmoja na miezi kumi, mkazi wa kijiji cha Nyankanga
wilayani Butiama.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara
ACP Paul Kasabago, amesema kuwa mtoto huyo alibakwa hadi kuvunjwa mguu
wake wa kushoto.
Mama mzazi wa
mtoto huyo Bi. Annaberi Waitara, akizungumzia tukio hilo akiwa Hopitali
ya Serikali Mkoa wa Mara Musoma, amesema kuwa mtoto wake alibakwa na
Shemeji yake huyo baada ya kumuachia wakati alipokwenda kuchota maji
kisimani.
0 Comments