Advertisement

Responsive Advertisement

NEWS ALERT: MADIWANI 6 WAVULIWA NYADHIFA ZAO HUKO KAGERA,WAMO CCM 5, MMOJA CUF


Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani Kagera imewavua udiwani madiwani sita 6 kati ya nane 8 wa manispaa ya Bukoba baada ya kupoteza sifa ya kuwa na nyadhifa hizo kutokana na utoro wa kutohudhuria vikao vya madiwani.


Mgogoro huo ulisababisha fedha za miradi ya maendeleo kurejeshwa serikali kuu bila kutumika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
Aidha madiwani hao hawataruhusiwa kugombea tena. Miongoni mwa madiwani hao 5 ni kutoka chama chama cha Mapinduzi na mmoja kutoka CUF

Ikumbukwe kuwa palikuwepo na mgogoro kati ya mbunge wa jimbo la Bukoba Balozi Khamis Kagasheki na aliyekuwa mayor wa manispaa hiyo Dr. Anathory Amani jambo lililosababisha madiwani wafuasi wa Kagasheki kususia vikao vya madiwani.

Na Hilali Ruhundwa- Malunde1 blog-Kagera

Post a Comment

0 Comments