Vikosi vya Ulinzi vya Kenya KDF
vimewapiga risasi watu watano wanaoshukiwa kuhusika na shambulio
lililotokea Mpeketoni katika eneo la pwani la Lamu hivi karibuni.
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Kenya imetangaza kuwa, washukiwa hao watano
walipigwa risasi na kuuawa wakati walipokuwa wakitoroka, ambapo
kumekamatwa pia silaha tatu aina ya AK-47.
Duru za jeshi la Kenya
zimeripoti kuwa, washukiwa hao watano wameuawa katika eneo la msituni,
wakati wa operesheni ya pamoja iliyolishirikisha jeshi na vikosi vya
usalama.
Katika miezi ya hivi karibuni Kenya
imeshuhudia milipuko ya maguruneti na mashambulizi ya silaha.Watu karibu
60 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulio mawili
yaliyofanyika hivi karibunikatika eneo la Mpeketoni, huko Lamu nchini
Kenya.

0 Comments